AfriKDP
Securing digital asset...
Please do not close this window
Non-Fiction - Business - Startups

Majira ya Damu na Usaliti

★★★★★No reviews yet
Instant DownloadGet access immediately
Secure CheckoutPowered by Paystack
Read AnywherePDF, eReader, Mobile
Creator SupportedDirectly supports the author

About This Book

Hadithi ya Usaliti na Mgogoro wa Kijamii. Dalain anagundua baba yake hakufungwa kwa bahati mbaya
majira damu na usaliti hadithi mgogoro

Kitabu hiki kinachunguza maisha ya Dalain, kijana anayepitia magumu ya maisha baada ya kupoteza familia yake. Anagundua ukweli kuhusu baba yake na siri zinazohusiana na usaliti na mgogoro wa kijamii.

Who this book is for

  • Wapenzi wa hadithi za maisha halisi
  • Wanafunzi wa biashara na usimamizi
  • Wale wanaopenda hadithi za usaliti
  • Wanaotafuta motisha katika maisha

What you'll learn

  • Kuelewa athari za usaliti katika jamii
  • Jinsi familia zinaweza kuathirika na matukio ya kihistoria
  • Mifano ya kujiinua kutoka katika hali ngumu
  • Mafunzo kuhusu umuhimu wa familia na urafiki
Read a free sample 3 pages from the book

MAJIRA YA DAMU NA USALITI (SEASON 01) Episode 01 Siku ya leo niliamka kama kawaida, baridi ileile, upepo uleule, na mwanga hafifu uliopenya, kuashiria kumepambazuka. Nilipofumbua macho, sauti ya swali lile lile likajirudia kama wimbo wa zamani usiokoma: “Nimekosea wapi?” Maisha yangu hayajawahi kubadilika. Kila siku Nimekuwa wa kurudia ile siku ya jana. Hakuna faraja mpya, hakuna habari njema, hakuna mtu wa kunikumbusha kuwa bado nina thamani duniani. Sina baba, Sina mama, Sina ndugu. Angalau niliwahi kuwa nao..... mapacha dada zangu wawili. Lakini sasa, wako wapi? Je, bado wako hai? Au nami nimesalia kuwa kivuli cha familia iliyosambaratishwa na majira ya damu na usaliti? Ninajiuliza pia... je, baba yangu anaweza kuwa hai mpaka leo? Kama yupo, anafahamu kuwa kuna mtoto wake anayeteseka mitaani? Au naye alizikwa zamani, Nakubakia tuu kumbukumbu za upendo wake? Nilinyanyuka taratibu kutoka kwenye “kitanda” changu sanduku la mabox lililotandikwa majani makavu kwaajili ya kuzuia baridi. Sina shuka. Sina blanketi. Marafiki nilionao usiku ni baridi kali na mbu wanaolia kana kwamba wanasherekea maumivu yangu. Nilikaa pembeni nikitazama juu kwenye anga lisilo na huruma, nikasikia pumzi yangu ikitetemeka. Maisha yangu ni magumu kuliko ilivyowahi kuwa. Na wakati mwingine najiuliza swali ambalo sijawahi kumwambia mtu yeyote:

“Mbona nimezaliwa? Kwa nini nimekuwa hivi?” Wakati nimeketi pale, nikihisi uchungu ukinipanda kama moto wa ndani, nilihisi machozi yanataka kushuka, nikayazuia. Mara ya mwisho kulia ilikuwa jana, na hiyo ilikua ni desturi yangu. Sikutaka kuyazoesha macho yangu machozi tena, Nilijitahidi kuyazuia. Maisha yangu yote nilikua nikioga kwa machozi au mvua za usiku na mchana. Siku zote wakati wa mvua kunyesha, sijawahi kuona sehemu salama ya kujificha mvua, niliogopa kujificha vibarazani kwa watu maana kwa muonekano niliokua nao ningeitwa mwizi. Leo nilishangaa sana sauti ikinirudia tena, Sauti inayonisumbua rohoni... Sauti ambayo sijawahi kuipa nafasi. Sauti iliyokuwa inaniambia: “Huu si mwisho... kuna kitu kinakuja.” Sikujua kuwa siku hii, ingekuwa mwanzo wa safari ambayo ingechora majira mapya, Majira ya maumivu, damu, na usaliti ambao dunia yangu haikuwa imewahi kuona. Siku iliofichua mengi ambayo yalikua kama giza kwangu licha ya kuzunguka kwa miaka mingi. Nikiwa nimeketi pembeni ya barabara, macho yangu yakiwa yamechoka na akili ikiwa imechoka pia kufikiria mambo yasiyojibiwa. Siku hii ikabadilika ghafla. Ilikuja kama upepo wa mbali sio mkali, sio mpole, lakini ule unaobeba ahadi na safari ya mabadiliko. Nilimuona bwana mmoja akipita na gari la kifahari, lenye rangi ya kung’aa isiyozoeleka mitaani. Alisimama taratibu karibu yangu, akashuka, na bila hata kuuliza sana akanipa shilingi elfu kumi. Nilishindwa kuamini. Sikuamini hata kama ni halisi. Sijawahi kupewa msaada wa pesa kubwa kiasi kile. Kwa sekunde chache nilijisikia kama Mungu alikuwa ameacha kuitazama dunia na ameangalia mahali nilipokaa mimi. Nilimshukuru sana, nikijisikia tumboni kama mtu aliyepata tumaini jipya baada ya wiki ndefu ya njaa. Lakini kabla sijamaliza hata mlio wa shukrani, aligeuka na kuniambia:

Itaendelea......... MAJIRA YA DAMU NA USALITI (SEASON 01) Episode 02 Nilimshukuru sana, nikijisikia tumboni kama mtu aliyepata tumaini jipya baada ya wiki ndefu ya njaa. Lakini kabla sijamaliza hata mlio wa shukrani, aligeuka na kuniambia: “Lakini.... Kijana... naomba tuongee kidogo.” Nilisimama. Nikamkaribia taratibu. Sauti yake ilikuwa na uzito wa mtu anayeona mbali zaidi ya macho. Aliniuliza mimi ni nani, Mbona ninaishi hapa, na familia yangu ipo wapi. Majibu niliyompa hayakua mepesi, yalikua makovu ya maisha. Nilimwambia ukweli bila kupunguza, bila kuongeza. Nilimwambia jinsi nilivyopotea, jinsi nilivyoishi mitaani, jinsi baba yangu alivyofungwa, na jinsi miaka ilivyopita bila hata kujua kama bado yuko hai. Nilimwambia natamani tu kupata nauli nirudi mji wa nyumbani nimuone baba yangu, nisikie sauti yake, au hata nisikie tu kama jina lake bado lipo kwenye orodha ya walio hai. Wakati nikiendelea kuzungumza, niliona uso…

End of sample. The full book is 34 pages on Afri KDP.

Questions about this book

Je, kitabu hiki kinahusiana vipi na biashara?

Ingawa ni hadithi ya kibinadamu, inatoa mafunzo muhimu kuhusu uongozi na ushirikiano katika biashara kupitia mfano wa baba wa Dalain.

Loading reviews...

Uncle J Library
Uncle J Library
Dar es salaam ~ Tanzania
1
Assets Published
0
Total Sales

Loading…

How do I get my book after paying?

A download link appears on this page as soon as your payment is confirmed, and a permanent copy of the link is emailed to you.

How do I pay?

By card from anywhere. In Nigeria you can also pay by bank transfer, USSD or mobile money. Your card details are entered on Paystack's secure page, never on AfriKDP.

Can I read it on my phone?

Yes. The file opens on phones, tablets, computers and eReaders.

Can I read it without buying it?

Yes, with an AfriKDP reading plan, which opens every book in the online reader and pays the author for every page you read.

What if something goes wrong?

Write to [email protected] with your email address and we will help. See our return policy.

Your Cart
—
—